Thursday, 31 May 2012

Video: Aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor ahukumiwa miaka 50 jela


Charles Taylor

**Shuka chini kwa video
Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.

Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa.

Mwandishi wa BBC aliyeko The Hague Anna Holligan anasema rufaa dhidi ya hukumu hii huenda ikachukua miezi sita. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu.

Child soldiers in Sierra Leone
Taylor pia alihukumiwa kwa kutumia watoto kama majeshi wakati wa vita huko Liberia

Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani.

Charles Taylor amelalamikia upande wa mashtaka kwa kuwatisha mashahidi katika kesi dhidi yake. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kwa kuwapa silaha waasi na kubadilishana na almasi.

Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.

Video:

Askofu Mokiwa acharuka Zanzibar

Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino Mokiwa


Rais wa Umoja wa Maaskofu Afrika Mashariki na Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Askofu Dk Valentino Mokiwa amesema waumini Wakristo hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi ukiwemo ufuatiliaji wa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa visiwani Zanzibar.

Akizungumza katika kikao kilichokutanisha viongozi wa Dini na Serikali katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais jana, Dk Mokiwa alisema Polisi imeshindwa kufuatilia matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuchomwa kwa makanisa hayo.

Alisema tangu mwaka jana zaidi ya makanisa 25 yamechomwa moto na hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani.

“Matukio mengi ya kuchomwa moto kwa makanisa yamejitokeza Zanzibar tangu mwaka jana lakini hakuna kesi iliyofikishwa mahakamani au mtu aliyekamatwa,” alisema Dk Mokiwa.

Aidha, alisema hadi sasa wafuasi Wakristo wanafanya kazi zao kwa hofu na wasiwasi kwani baadhi ya watu bado wanashambulia nyumba za ibada ikiwa ni pamoja na kurusha mawe.

“Hadi sasa wafuasi wetu wanafanya kazi zao kwa wasiwasi mkubwa hata katika nyumba za ibada kwani wafuasi wenye siasa kali wanarusha mawe katika nyumba za ibada,” alisema.

Dk Mokiwa alisema hakubaliani na kauli za baadhi ya watu kwamba wanaofanya vitendo hivyo ni wahuni, bila hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao.

Alifafanua, kuwa kama ni suala la Muungano kwa nini watu hao wachome moto makanisa na wasisubiri Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba ili wawasilishe hoja zao kuhusu Muungano.

“Sisi hadi sasa hatuamini kwamba wanaofanya fujo ni wahuni, kama ni wahuni kwa nini wanachoma moto makanisa na kama ni Muungano kwa nini wasisubiri Tume ya Katiba? “Alihoji Askofu Mokiwa.


Askofu Mkuu wa Tanzania Dk.Mokiwa akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud, walipofika Ofisi hapo kwa ajili ya mazungumzo na Waziri kuhusiana na vurugu zilizoyokea wiki iliopita na kusababisha uharibifu na uvyunjaji wa makanisa katika sehemu mbalimbali na mali za baadhi ya wananchi kuharibiwa

Mapema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akijibu baadhi ya hoja za Baraza la Maaskofu Tanzania, alisema tayari Serikali imeweka ulinzi wa kutosha kwa makanisa yote visiwani hapa.

“Tumeweka ulinzi katika sehemu zote za nyumba za ibada ikiwamo makanisani na Serikali itahakikisha hakuna fujo zitakazojitokeza kwa sasa,” alisema Aboud.

Aliahidi kuwasilisha kwa Rais Dk Ali Mohamed Shein malalamiko yao yote kuhusu vitendo vya kuwadhalilisha Wakristo visiwani huku Tanzania ikiwa nchi isiyo na dini isipokuwa wananchi.

Mapema viongozi hao walitaka kuonana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ) kuzungumzia matukio hayo yenye kuashiria uvunjifu wa amani na utulivu.

Hata hivyo Aboud alikiri akisema wapo watu wanatumia vibaya taasisi za kidini kama mwamvuli wa kisiasa katika kuwasilisha hoja zao mbalimbali, yakiwamo masuala ya Muungano na marekebisho ya Katiba.

Jacquline Wolper: "nilikuwa nikiupenda Uislam na kuweka picha zenye viashiria vya dini hiyo ndani kwangu"



Nyota wa kike anayetamba ndani ya Bongo Movies, Jacqueline Wolper ameweka wazi ya kuwa dini ya Kiislam ameipenda siku nyingi kabla hajakutana na mpenzi wake Dallas.

Wolper alizungumza hayo kupitia kwenye TV ya Channel Five pale alipoulizwa kama alibadili dini kwa sababu ya mpenzi wake huyo wa sasa. Lakini mrembo huyo alipinga suala hilo na kusema alikuwa akiuupenda uislamu kabla hata hajakutana na Dallas.

“Nakumbuka nilikuwa nikiupenda Uislam na kuweka picha zenye viashiria vya dini hiyo ndani kwangu hivyo Dallas alinikuta tayari ninapenda ndipo nikabadili,” alisema Wolper.

Wednesday, 30 May 2012

Picha: Wema Sepetu avishwa pete ya uchumba


Wema mwenyewe original


Sam Machozi, Snura & Sharo Millionaire



Jamillar, Chaz Baba & Snura in da house


Wema akiwa na mlinzi wake


Wema akila pozi na Abou



DJ Choka akiwa kapozi na Wema Sepetu


Mwinyi wa Machozi Band akiproposal kwa Wema



Ombi harimae limekubaliwa



Pete ikawekwa kwenye kidole sahihi



Si unajua tena mambo ya furaha


Kwa picha zaidi tembelea: Bongo Star Link

Tuesday, 29 May 2012

Chama cha CUF chalaani vitendo vilivyotokea vya uvunjaji amani Zanzibar




THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)

Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk Homepage: www.cuftz.org


Our Ref: CUF/HQ/ONKM/U/003/2012/13 Date: 29/05/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Umma unashuhudia hali tete ya machafuko ambayo hayakutarajiwa yakiibukia tena Zanzibar, wakati ambapo Nchi ilishaanza kunawiri matunda ya utulivu na maridhiano, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Pamoja na sababu au visingizio mbali mbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwamo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hikma, matumizi ya nguvu za dola, na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutopendelea Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar.

Kwa thamani yoyote hakuna asiyeweza kubaini umuhimu wa hali ya amani na utulivu, na madhara ya kukosekana kwake, hasa katika Visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambavyo vimewahi kuelemezewa athari kubwa ya machafuko kwa muda mrefu.

Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania, hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo, kwa maslahi binafsi, na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa.

Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao.

Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi.

Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE


…………………………………….
Salim A Bimani
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma

Mambo hayo: Woman Marries Herself

woman marries herself nadine schweigert


Nadine Schweigert married herself in a beautiful ceremony attended by 300 guests.

The 36-year-old divorced mom of three wore blue satin and clutched a bouquet of white roses as she walked down the aisle before a gathering of 45 friends and family members in Fargo, North Dakota.

She vowed to "to enjoy inhabiting my own life and to relish a lifelong love affair with my beautiful self," reports Fargo's InForum newspaper . After the ring was exchanged with the bride and her inner-groom, guests were encouraged to "blow kisses at the world," and later, eat cake.

Schweigert, who followed the ceremony with a solo honeymoon in New Orleans, claims the wedding was her way of showing the world she's learned to love and accept herself as a woman flying solo.

"I was waiting for someone to come along and make me happy," she said." At some point, a friend said, 'Why do you need someone to marry you to be happy? Marry yourself.'"

Woman Marries Herself

Not everyone was in agreement. Some of Schweigert's friends, who'd undoubtedly seen Carrie Bradshaw register for a pair of Manolos on season 6 of Sex and the City, thought she was going a little far with the single pride thing. Schweigert's 11-year-old son was her biggest critic: "He said, 'I love you, but I'm embarrassed for you right now.'"

Some feel that the idea is a bad one. "Marriage is about union, it's about partnership, most of all, it's about compromising on and sharing the things in your life that are hard to compromise on or sharp to deeper, more personal elements like beliefs, emotional vulnerabilities, and bank accounts," said Cindy Rosen.

Self-marriage, to some, is an oxymoron. Singlehood means freedom, marriage means enclosure. Both can have serious value and can be cozy and wonderful, but getting married to yourself feels strange to most. Why not just embrace the glory of being single and live an awesome life full of not fighting over the covers or smelling someone else's weird smells? And have a party to celebrate it! To support this, I will show up and buy you two blenders, a rice cooker, a lacy keepsake frame, and small towels you don't know what to do with.

But if you marry yourself, you have a great chance of making it last -- forever

Video; why she did that:

Wamarekani weusi wabanwa na sheria mpya za uchaguzi

Rep. Emanuel Cleaver (D-MO)















Rep. Emanuel Cleaver Mjumbe wa Baraza la Congress (CBC).

Wajumbe Weusi katika Baraza la Congress (CBC) nchini Marekani wameitisha mkutano wa kitaifa kujadili sheria mpya za kadi za kupigia kura ambazo zinaonekana kuwadhoofisha wapiga kura weusi au wenye asili ya Afrika nchini humo.

Press TV imeripoti kuwa, huenda idadi kubwa ya Wamarekani weusi wakashindwa kupiga kura katika uchaguzi wa rais mwezi Novemba kutokana na sheria ambazo zimepitishwa katika majimbo kadhaa. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kila mpiga kura anapaswa kuwa na kadi maalumu ya upigaji kura katika hali ambayo huko nyuma kura zimekuwa zikipigwa bila kadi hiyo.

Taasisi ya Utafiti ya Brennan Center imesema sheria ya kadi ya kura itawaathiri vibaya Wamarekani weusi. Aidha baadhi ya majimbo ya Marekani yamepitisha sheria za kubana harakati za kushajiisha uandikishaji wapiga kura zilizokuwa zikitekelezwa na makundi ya wanawake na Wamarekani weusi.

Zungu lakamatwa likiiba pesa kutoka katika ATM Dar



Habari kamili: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/mzungu-adakwa

Mtoto aliyezaliwa na miguu sita afanyiwa upasuaji uliofanikiwa


Kitoto kilichozaliwa na miguu sita

MTOTO mmoja amezaliwa jijini Karachi nchini Pakistan akiwa na miguu sita na amefanyiwa upasuaji kuondoa iliyozidi.

Jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji huo Alhamisili iliyopita kwenye taasisi iitwayo National Institute of Child Heath (NICH), jijini Karachi wamesema upasuaji ulikwenda vizuri kama walivyopanga.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Dk. Jamal Raza ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa NICH, alisema miguu mingine iliondolewa kwa operesheni na hali hiyo hutokea mara chache sana.



“Kati ya watoto milioni moja, anaweza kutokea mmoja tu kukumbwa na hali hiyo kutokana na maradhi ambayo kitaalamu huitwa Genetic Disease. Mtoto huwa si wa kawaida,” alifafanua Dk. Raza.

Alisema mtoto huyo kabla hajafanyiwa upasuaji alipimwa na kipimo maalum, CT Scan ndipo walipoamua kumfanyia upasuaji uliochukua saa nane.

Baba wa mtoto huyo ambaye hajapewa jina, Imran Shaikh, alisema ameshukuru mtoto wake kupata tiba hiyo na sasa amekuwa kama watoto wengine.

 “Sisi ni maskini, naishukuru serikali kwa kusaidia tiba ya mwanangu,” aliwaambia wanahabari.

Elizabeth Michael "Lulu" afikishwa mahakamani, lakini umri wake bado ni kitendawili

Lulu akijaribu kutabasamu mbele ya kamera

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.

Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.

Lulu akiteremka kutoka ndani ya basi la magereza

Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.

Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.

Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.

Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.

Lulu akiwa mahakamani huku akionekana anafikiria kitu


Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.

Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.





Ulinzi jinsi ulivyokuwa mkali mahakamani hapo

Baba yake Lulu (kushoto) akiwa na wakili Kennedy Fungamtama anayeliongoza jopo linalomtetea msanii huyo.

Source: Global pulishers

Monday, 28 May 2012

Picha: Yaliyotokea Zanzibar siku ya Jumapili tarehe 27/05/2012

Moja ya gari zilizoathirika kwa uchomwaji moto


Kikosi cha Zimamoto kikijaribu kuudhibiti moto uliokuwa ukiinguza gari


Wananchi wakiangalia mambo yaliyojiri


Moto ulikuwa ukiwa umeanzishwa sehemu mbalimbali




Polisi wakiwa tayari kwa lolote
 

Darajani kulikuwa hakuna biashara

 
Matairi ndio yaliyotumika kuwashia moto
 
Source: ZanziNews

Sunday, 27 May 2012

Taarifa Rasmi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kwa Wananchi Kuhusu Maandamano na Matukio ya Uvunjifu wa Amani

Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar.
---
Itakumbukwa kwamba tarehe 25 Aprili, 2012 Kamati Maalumu ya Mawaziri ilikutana na viongozi wa jumuiya ya Uamsho, Maimamu na Masheikh kuzungumzia hali iliyojitokeza nchini katika kufanya mihadhara ambayo ilikuwa inaashiria uvunjifu wa amani.

Katika kikao hicho Serikali iliwataka Viongozi hao wanapofanya mihadhara na mikutano inayohusu masuala ya maoni ya katiba wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.

Aidha, Serikali iliwasihi viongozi hao kuepuka matumizi ya lugha na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika nchi yetu na iliwataka pale ambapo wana maoni yoyote kuhusu Serikali wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali itakuwa tayari kuzungumza nao ili kuwa na mustakabali mwema katika nchi yetu.

Vile vile, kupitia taarifa maalumu ya Serikali iliyotolewa Aprili-Mei mwaka huu, Serikali ilieleza wazi kwamba tume ya marekebisho ya katiba imezinduliwa rasmi na kuwataka wananchi, taasisi na vikundi mbali mbali nchini vyenye nia ya kutaka kuelimisha umma kuhusu marekebisho ya katiba kufuata muongozo wa sheria namba 8 ya mwaka jana kama ilivyorekebishwa na sheria namba 2 ya mwaka huu 2012.

Kwenda kinyume na sheria hii ni kosa la jinai na hivyo iliwataka Wananchi wote kujiepusha na vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na matakwa ya sheria.

Ndugu Wananchi, mbali na juhudi hizo za Serikali, bado wapo watu wachache wasioitakia mema nchi yetu na umoja uliopo wanaendeleza kwa makusudi vitendo vya kuvunja taratibu za sheria jambo ambalo limepelekea Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria.

Ndugu Wananchi, Serikali imesikitishwa na vitendo vilivyojitokeza vya vurugu na uvunjifu wa amani ambavyo vimeelezwa kwa kina na Jeshi la Polisi iliyotolewa mapema leo tarehe 25.05.2012 na Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kutokana na hali hiyo, Serikali inawahakikishia Wananchi wote kwamba itaendelea kudhibiti vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria vinavyoashiria kuondolea nchi yetu amani na utulivu uliopo.

Ndugu Wananchi, Serikali inawahakikishia Wananchi kwamba Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua zifaazo ili kuwahakikishia usalama wa raia na mali zao unakuwepo na hali inaendelea kuwa shuwari, amani na utulivu.

Ndugu Wananchi, bado Serikali inasisitiza na kuwaomba wananchi wote waunge mkono juhudi za Serikali na kuacha kabisa kujiingiza katika vitendo ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani na utulivu katika nchi yetu.

Hivyo, tunawaomba Wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na Serikali itaendelea kuwahakikishia usalama wao.

Aidha, Serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao wasijiingize katika vitendo viovu na vurugu kwani Jeshi la Polisi na Vikosi vyote vya Ulinzi na Usalama vitakuwa macho kupambana na vurugu hizo na vitendo vyote vya uvunjifu wa amani.

Kwa madhumuni ya kudhibiti amani na utulivu na usalama wa Wananchi wetu, Serikali katika kipindi hiki itachukua hatua zifuatazo:
  1. Inakataza mikusanyiko ya aina mbalimbali, maandamano, na mihadhara ya aina mbalimbali ambayo haijapata kibali cha Serikali.
  2. Serikali inaliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na kufanya fujo zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar
  3. Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa amali zilizofanywa katika taasisi za umma, dini na mali za watu binafsi.
  4. Serikali inawapa pole Wananchi na Taasisi zilizoathirika na vurugu hizo na kuwahakikishia kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika katika kadhia hiyo.

Na mwisho, tunawaomba wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ahsanteni.

Nawashukuru kwa kunisikiliza.


Mohammed Aboud Mohammed,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Zanzibar.

Saturday, 26 May 2012

Video: Polisi waliokamatwa kwa kuomba rushwa katika barabara ya Nairobi - Nakuru wafikishwa mahakamani


Maafisa wanne wa polisi wa idara ya trafiki waliokamatwa kwa madai ya ulaji wa hongo kutoka kwa madereva wanaotumia barabara ya Nairobi-Nakuru katika mwaka wa 2010 wamefikishwa mahakamani leo (jana) huko Nyeri.

Maafisa hao wanne walikamatwa na maafisa wa tume ya kukabiliana na ufisadi katika tukio ambalo liliwaacha wakenya vinywa wazi walipozitazama picha za video zilizopeperushwa kwenye vyombo vya habari wakati huo.

Washukiwa hao wanatarajiwa kufika mbele ya hakimu mkuu wa nyeri Evans Makori mwezi ujao Juni.

Nyumba Yateketea kwa Moto huko Fuoni Kijito Upele


Wananchi wakiangalia Nyumba ilioteketea kwa moto katika maeneo ya Kijito Upele


Watu watatu wamenusurika kufa baada ya nyumba waliokuwa wamelala kuteketea kwa moto, huko Fuoni Kijito upele Mkoa wa Mjini Magharibi.


Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo moto huo uliteketeza kila kitu ndani ya nyumba hiyo, na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.


Akizungumza mama mwenye nyumba hiyo Khadija Mohammed, alisema akiwa amelala na wenziwe wawili, ndipo walipoushuhudia moto huo ukiteketeza nyumba na kuamshana.


“Ilikuwa usiku baina ya saa 7:30 hadi saa 8:00 tukiwa tumelala wakati natoka nje, niliona moto huo unawaka ndipo nilipowaamsha na kutoka nje, hatukuwahi kutoa kitu chochote ndani’’,alisema.


Akitihibisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi Mkoa Kusini Unguja kamishina msaidizi wa polisi, Augustine Ollomi, alisema kuwa chanzo cha moto huo hadi sasa bado hakijajulikana na jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi ili kufahamu chanzo chake.


Kamanda Ollomi aliwataja watu hao walionusurika kufa ni Khadija Mohammed (47), Abubakar Othman (17) na mmoja alitajwa kwa jina moja Rajabu, huku mmiliki wa nyumba hiyo akiwa ni Ajuwedi Mohammed Ajuwedi (40), ambapo wakati wa tukio hakuwepo.
 
 


Aidha kamanda huyo alivitaja baadhi ya vitu ambavyo vilikuwemo ndani ya nyumba hiyo kuwa ni vespa moja, Friji, baskeli, nguo za aina mbali mbali majiko ya umeme pamoja samani mbali mbali, ambapo hadi sasa hasara kamili haijajulikana.


Hata hivyo Kamanda huyo alisema kuwa hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa, mbali hasara ya vitu iliyopatikana.
 
Source: ZanziNews

Video: Wabunge wachapana bungeni huko Ukraine, kisa matumizi ya lugha


Ngumi mtu ndani ya bunge

Wabunge nchini Ukraine waliamua kuzichapa ndani ya kikao cha bunge baada ya wabunge hao kukosana juu ya matumizi ya lugha ya Kirusi katika sekta serikali.

Mjadala katika bunge la Ukraine kuhusu sheria ambayo ingeruhusu lugha ya Kirusi kutumiwa katika mahakama, hospitali na taasisi nyingine katika maeneo ya Urusi ambayo wakazi wake wanazungumza Kirusi umesababisha bunge hilo kugeuka kuwa jukwaa la masumbwi baada ya wanasiasa kurushiana ngumi.




Wabunge wa chama cha rais Viktor Yanukovich wanataka lugha ya Kirusi ikubaliwe kama lugha rasmi ya pili nchini humo, lakini upinzani unaounga mkono sera za magharibi unapinga sheria hiyo.

 
Kufuatia tafrani huyo ya kupigana ilibidi mbunge mmoja wa upinzani apelekwe hospitali baada ya purukushani hiyo.


Video:

Hospitali ya Mnazi Mmoja yaelemewa na wajawazito



Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja mjini hapa, imezidiwa na idadi kubwa ya akinamama wanaokwenda kujifungua, na hata kusababisha watoto wanaozaliwa kulazwa watatu katika kitanda kimoja.

Katibu wa Hospitali hiyo, Omar Abdalla alikiri kuwepo kwa idadi kubwa ya akinamama wanaojifungua katika hospitali hiyo na hivyo kuzidiwa.

“Ni kweli hospitali imezidiwa na idadi kubwa ya akinamama wanaofika hapo kujifungua ambapo kitanda kimoja kinatumiwa kulaza watoto watatu,” alisema.

Alizitaja baadhi ya sababu zilizopelekea hospitali hiyo kuzidiwa na idadi kubwa ya akinamama wanaokwenda hapo kwa ajili ya kujifungua kwa imani kwamba watapata huduma nzuri za uhakika.

“Hospitali ya Mnazi Mmoja ni ya rufaa kwa hivyo watu wengi imani yao kubwa kwamba watapata tiba nzuri na salama,” alisema.

Akifafanua zaidi, alisema mkunga mmoja wa hospitali hiyo anawahudumia wajawazito zaidi ya 13 kwa siku wakati katika hospitali za Fuoni na Mwembeladu, mkunga mmoja hutoa huduma kwa akinamama wapatao watatu kwa siku.

Friday, 25 May 2012

Diamond: “Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate"


Jokate Mwegelo

Ile kashfa ya Diamond kunaswa hotelini na mcheza sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel inadaiwa kuchafua vibaya upande wa wakwe zake Diamond.

Mtu wa karibu wa pande zote hizo mbili alisema: “Asikwambie mtu, unajua upande wa akina Jokate ni watu wa dini sana. Yaani kwa skendo skendo kama hizo, wanamuona Diamond kama anataka kuwachafua.

“Unajua zile ishu za kudaiwa kutoka kimapenzi na msururu wa wanawake zilikuwa zimeanza kutulia kwa sababu yupo na Jokate lakini baada ya kutokea hii ya kunaswa hotelini na Aunt, imetibua mambo kule ukweni na mbaya zaidi anaonekana hajatulia,” alimalizia mtu huyo ambaye hakutaka jina lake liwekwe hadharani


Diamond

Baada ya habari hizo kutufikia tuliamua kumtafuta Diamond kuthibitisha juu ya hayo yaliyozungumzwa. Alipopatikanwa alikuwa na haya ya kusema: “Naomba niweke wazi jambo hili kwa sababu ni kweli nachafuliwa.

“Kuna watu wananichafua ili nionekane kituko kwenye familia ya akina Jokate, nahisi wanaweza kufanikiwa,” alisema Diamond.

Kufuatia ishu hiyo, uhusiano wa kimapenzi wa mwanamuziki huyo Diamond na mwanamitindo Jokate unadaiwa kuwa kwenye hatihati pamoja na kwamba bado wapo pamoja.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond na Aunt walidaiwa kukutwa katika Hoteli ya Kebby’s iliyopo Mwenge, jijini Dar wakila ‘good time’, hivyo kuzua tafrani kwenye uchumba wa mwanamuzi huyo na Jokate.