Friday, 24 May 2013

Hatimae Jumuiya ya Annoor Leicester wafanikiwa kupata jengo


  • Mchango wako unahitajika



Assalaamu Alaykum Wa Rahmatul Laahi Wa Barakaatuh

(Registered Charity Number: 1146906)

Alhamdulillaah, Jumuia ya Annoor (madrassatul Noor Leicester) ya Uingereza ina furaha kuujulisha Umma wa Kiislamu kuwa imefanikiwa kwa uwezo wa Allah kusaini mkataba wa kukodi jengo kwa ajili ya shughuli za Kiislamu zikiwemo Msikiti, Masomo ya Dini na shughuli nyingine za Kiislamu.

Hii ni hatua ya awali na muhimu katika kufanikisha kulinunua jengo hilo.

Mkataba umetiwa saini siku ya Jumatatu 17 Mei 2013.

Jengo lipo kati kati ya mji wa Leicester ( Leicester City Centre)

Thamani yake ni £175,000.

Shukrani za dhati kwa kila aliyechangia kwa mali, ushauri na Dua, Allah akulipeni kila la heri, Amin.

Mchango wenu bado unahitajika ili kukamilisha manunuzi ya jengo, ambapo tuna muda wa mwaka mmoja na miezi 9 kukamilisha.

Kumbuka muislamu, unachotanguliza mbele ya Allah basi hakika utakikuta maradufu!!!

Tunakaribisha michango yenu kupitia akaunti ya Jumuia hapo chini:

Account Name:                Madrassatul Noor Leicester

Bank:                                 Lloyds TSB, Town Hall Square, 17 Horsefair Street, Leicester, LE1 5PD

Account Number:            45127768

Sort Code:                         30-94-97

IBAN:                                  GB27LOYD30949745127768

SWIFT BIC:                         LOYDGB21029

Wabillahi Tawfeeq

Mohammed Omar
Mwenyekiti,
Annoor Community Centre, 170a Belgrave Gate, Leicester, LE1 3XL

Wednesday, 29 August 2012

Video: Watoa sharti la kuruhusiwa kula nyama ya Punda ili wakubali kuhesabiwa huko Arusha


Sensa ya mwaka huu nchini Tanzania imekumbwa na mambo kibao. Ikiwa baadhi ya waislamu nchini humo wakikataa kuhesabiwa kwa sababu zao fulani.

Huko nchini Arusha kuna baadhi ya watu sharti lao lilikuwa waruhusiwe kula nyama ya Nyani na kunywa gongo au waruhusiwe kula nyama ya Punda. Hivyo serikali katika kufanikisha zoezi la uandikishaji ikaona bora watoe ruksa ya wananchi hao kula nyama ya Punda.

Kenya PM blames killing of Muslim cleric on nation's foes

Civilians carry the body of Aboud Rogo Mohammed along the Mombasa-Malindi highway in Kenya's coastal city of Mombasa August 27, 2012. REUTERS/Joseph Okanga
Civilians carry the body of Aboud Rogo Mohammed along the Mombasa-Malindi highway in Kenya's coastal city of Mombasa August 27, 2012.

Kenya's prime minister said on Wednesday the country's enemies were behind the killing of a Muslim cleric that triggered riots he described as being conducted by an "underground organisation" to create divisions between Christians and Muslims.

Aboud Rogo, accused by the United States of helping al Qaeda-linked Islamist militants in Somalia, was facing charges in a Kenyan court of possessing weapons when he was shot in his car by unknown attackers in Mombasa on Monday.

His death unleashed two days of riots in which five people, including three police officers, were killed.

A measure of calm has returned to Kenya's second-biggest city, a tourist hub and major Indian Ocean port, as anti-riot police armed with wooden batons, teargas and automatic rifles patrolled its busy streets.

"We suspect the hand of the enemies of our country in this, those who want to create religious animosity," Prime Minister Raila Odinga told reporters after addressing religious leaders in the city.
"It is an attempt to try create a division between Christians and Muslims in our country so that it appears it is a religious war."

He said Kenya had many enemies, including abroad, after it sent troops into neighboring Somalia last October to fight Islamist militants.

Asked whether the violent reaction in the streets of Mombasa, which has a big Muslim minority, was organized or just a spontaneous outpouring of anger the prime minister said: "Certainly, that is what it looks like."

"Why deliberately attack churches? That must be part of an organized (reaction). Where did the grenades come from? It confirms our suspicions that there is a serious underground organisation conducting this," he said.

Rioters set fire to at least six churches, stoking fears that the unrest may become more sectarian in a city where grenade attacks blamed on Somali militants and their sympathizers have already strained Muslim-Christian relations.

CHURCHES BURNT

The National Council of Churches of Kenya, said in a statement it had followed with "growing trepidation" the increasing attacks on Christians and churches.

"The violence appears well planed, pre-meditated, and systematic. In the last five months alone, 11 churches have been attacked while attempts were made on others," the group's general-secretary, Peter Karanja, said.

"Christians have been killed, injured or maimed for life. We see this as an intentional provocation of Christians to retaliate."

On Tuesday, mobs of youths fired machineguns at police in Kisauni, a predominantly Muslim area, just before throwing a grenade into a police truck, police said. Two Kenyan police officers and a civilian were killed instantly.

One more police officer died on Wednesday of wounds inflicted in the grenade blast. One person was killed when the riots broke out on Monday.

Some 24 people arrested during the riots were charged in a Mombasa court On Wednesday for assembling illegally and they were remanded in custody for five days.

Police said they were likely to add more charges of arson and destruction of property.

Residents, however, accused the police of being heavy-handed, especially in Majengo, another neighborhood with a large Muslim population that had been one of the flashpoints of violence. Locals were ordered by police to stay in their houses.

"It is getting better, but police should stop intimidating people. I closed my shop the whole of yesterday. Today am open but still very careful. I hear any noise I close immediately," said Margaret Mumo, owner of a chemist shop at Sabasaba, near Majengo.

Polisi Tanzania wawakamata waliokataa kuhesabiwa


Miji mbalimbali ya Tanzania imeshuhudia oparesheni kali ya inayoendeshwa na polisi kwa lengo la kuwakamata watu wanaotatiza zoezi la kuwahesabu watu linaloendelea.

Habari zaidi zinasema kuwa tayari watu kadhaa wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kukataa kuhesabiwa. Viongozi wa Kiislamu wilayani Muheza wamehojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani humo kwa tuhuma za kuwashawishi wananchi wasishiriki Sensa.

Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu amesema amewaita viongozi hao wa dini kutokana na matamshi yao ya kuwahamasisha wananchi wasishiriki Sensa. Mkoani Kigoma, polisi wamewakamata na kuwafungulia mashtaka watu 12 kwa kosa la kukataa kuhesabiwa. Watu hao wamedai kuwa mila na desturi zao haziruhusu binadamu kuhesabiwa kama wanyama.

Sensa ya watu na makazi iliyoanza Agosti 26, imekumbwa na changamoto nyingi huku Waislamu wakitakiwa kulisusia zoezi hilo baada ya serikali kukataa kuorodhesha suali la dini katika madodosa ya sense hiyo.

Sensa ya mwaka 2002 ilionyesha kuwa idadi ya Watanzania ilikuwa takriban milioni 34.5 na inatarajiwa kwamba idadi ya watu kwenye sense ya mwaka huu huenda ikapindukia milioni 40.

Tuesday, 28 August 2012

Babu wa Loliondo kumbe ni TAPELI


Babu akitayarisha dawa yake kwa mamilioni waliofika kupata kikombe

SERIKALI imethibitisha kuwa kitendo alichokuwa akifanya babu wa Loliondo, Mchungaji Ambilikile Masapile, cha kutoa dawa ya kutibu magonjwa, ukiwemo Ukimwi aliyokuwa amedai kuwa ameoteshwa na Mungu ni cha kitapeli.

 Utafiti umebaini kwamba dawa hiyo ya babu wa Loliondo ni feki na kwamba haina uwezo wa kutibu Ukimwi wala kisukari.

Kwa mujibu wa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi (pichani), utafiti wa kulinganisha wagonjwa wa Ukimwi na kisukari waliokunywa dawa hiyo na wale ambao hawakunywa, umebaini kwamba hakuna utofauti wa afya ya mgonjwa.

Alisema utafiti huo unafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), ulianza Machi mwaka huu na kwamba unahusisha wagonjwa 200 wanaofuatiliwa kwa kupimwa damu, kinga ya mwili (CD4) na uzito wa mgonjwa, ambao ulifanyika tangu mgonjwa alipokunywa kikombe cha babu.

“Matokeo ya awali ya utafiti yameonyesha kuwa hakuna utofauti katika vipimo vya kimaabara pamoja na damu, CD4, uzito na ubora wa afya ya wagonjwa kati ya waliokunywa na wale ambao hawakunywa dawa ya mchungaji,” alisema Dk. Mwinyi.

Alisema lengo la utafiti huo ni kubaini uwezo wa dawa hiyo katika kutibu magonjwa aliyosema dawa yake inayatibu ili kuona kama kuna utofauti wowote baada ya mgonjwa kutumia dawa.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini limesema kwamba linafuatilia kwa makini sakata la Mchungaji Masapile anayeishi katika kijiji cha Samunge mkoani Arusha kufuatia malalamiko ya wananchi kuwa licha ya dawa yake kuonekana haitibu, bado watu wanakwenda na kunywa.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni ofisini kwake makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, amesema kwamba kutokana na malalamiko hayo polisi watawasiliana na wizara ya afya ili kuchukua hatua stahiki.

Msemaji huyo amesema kwamba wanataka kujua kama wizara ya afya imepiga marufuku dawa hiyo au inasema nini baada ya kubainika kuwa haitibu na amewataka wananchi kutoenda huko.

 Wananchi wengi waliozungumza na gazeti hili wamedai kwamba Babu amewatapeli wananchi na kinachowauma ni kuona kuwa kuna watu wanaendelea kwenda kunywa kikombe japokuwa hawatangazwi.

“Wananchi wengi waliuza mali zao na kukimbilia kwa babu kupata tiba, kumbe ulikuwa ni utapeli, ukweli ni kwamba serikali imechelewa mno kutoa tangazo hili,” alisema mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la John.

Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyama vya Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi nchini (TAMOPHA), Julius Kaaya, ameitupia serikali lawama kwa kuipigia debe dawa ya Babu na kuwafanya wagonjwa kutoroka hospitali huku wengi wao wakiacha kuendelea na dawa wakiamini wangepona baada ya kunywa kikombe kimoja .

“Huyu Babu inatakiwa ashitakiwe apelekwe mahakamani afilisiwe mali zake zote alizochuma toka kwa wagonjwa na ikiwezekana afungwe ili iwe fundisho kwa watu wengine,” alisema Kaaya na kuongeza kuwa wao wanajiandaa kumfungulia kesi.

Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste (TAG) Mkoani Arusha, Steve Wambura, amemtaka babu huyo amrudie Mungu kwa kutubu kuwa aliwatapeli wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Waganga wa Tiba Asili Mkoa wa Dar es Saalam, Maneno Tamba, amesema babu huyo siyo mwanachama wao na walishangazwa na serikali kumpigia debe, hali iliyosababisha vifo vya watu wengi waliomkimbilia na kuacha tiba sahihi.

Baadhi ya mawakili, akiwemo Mabere Marando wamesema kwamba wapo tayari kumfikisha mahakamani babu huyo wakijitokeza waliotapeliwa na watamfungulia kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Monday, 27 August 2012

Ghasia zazuka Mombasa baada ya Aboud Rogo kuuawa


Sheikh Aboud Rogo baada ya kuuliwa kwa risasi ndani ya gari lake


Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya muhubiri wa kiisilamu ambaye pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa risasi mjini Mombasa Kenya.

Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa katika mtaa wa Majengo kufuatia makabiliano kati ya polisi na mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa

Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga maduka yao na watu kukimbilia usalama wao katika mtaa wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini Mombasa.

Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini katika mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.

Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.

Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita, alizikwa baadaye saa za mchana.

Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.

Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini Somalia la al-Shabab

A policeman guards the van in which Aboud Rogo Mohammed was shot and killed in, along Mombasa Malindi highway in Kenya’s coastal city of Mombasa. (Reuters)
Polisi wakilinda gari ambalo ndilo alilokuwa akiendesha Aboud Rogo na kuuliwa akiwa ndani ya gari hilo


Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.

Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.

Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.


Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi hilo kwa vifaa vya kisasa.

Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.

Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Thursday, 23 August 2012

Picha: Dereva wa gari anusurika kifo kimiujiza baada ya gari yake kuangukiwa na lori China

Click the image to open in full size.
Lori linavyoonekana baada ya kuliangukia gari dogo

Click the image to open in full size.
Askari wa zimamoto na baadhi ya raia waijitahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya dereva kwenye gari dogo lililoangukiwa na lori

Click the image to open in full size.
Hatimae Lori limefanikiwa kuinuliwa, na sasa kazi ilikuwa kumtoa dereva

Click the image to open in full size.
Watu wa zima moto na watu wa huduma ya kwanza wakiwa wanahangaikia katika kuokoa dereva huyo

Click the image to open in full size.
Click the image to open in full size.
Hatimae dereva afikiwa na bado akiwa hai.

Sunday, 19 August 2012

Picha: Sala ya Eid katika jiji la Leicester nchini Uingereza

Waumini wa kiislamu Leicester wakisubiri sala ya Eid kusaliwa
 
Sheikh Saleh Juma akikumbushia suala la Zakatul Fitr kabla ya sala kuanza
 
Sheikh Abdalla Sane aijiandaa kwenda kusalisha sala ya Eid iliofanyika katika ukumbi wa Taylor Road School
Imam akisisitiza juu ya safu kuwa sawa kabla ya sala
Hatimae sala ikasliwa kwa salama na amani
 
Sheikh Abdalla Sane akitoa hotuba ya sala
Mwenyekiti wa An Noor Community Leicester Mohd Omar (mwenye koti) akiwa makini katika kufatilia hotuba
 
Kila mtu alikuwa makini katika hotuba hiyo

Mwenyekiti wa An Noor akihamasisha juu ya mchango wa jengo ambalo jumuiya ipo katia harakati ya kulinunua

Inshaallah hawa ndio wanafunzi watakaonufaika na jengo hilo ambalo jumuiya ya An Noor inalipigania kulipata
Kama kawaida ya kila Eid watu wote walikusanyika pamoja na upata kifungua kinywa katika jengo letu la chuoni


Baadhi ya wajumbe wa An Noor Community Leicester baada ya kukamilisha shughuli yote ya suala zima la Eid

Thursday, 19 July 2012

Picha: Shughuli ya kuzika maiti zilizopatikanwa kutoka katika ajali ya meli Zanzibar


Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.


Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.


Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.
Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.


Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.

Source: ZanziNews

Wednesday, 18 July 2012

Nelson Mandela atimiza miaka 94


Aliyekuwa Rais wa Marekani Bill Clinton alipomtembelea aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini hapo jana huko nyumbani kwake Qunu, South Africa's Eastern Cape Province.

Bwana Nelson Mandela leo (18th July 2012) ametimiza miaka 94 ya kuzaliwa.

Tuesday, 17 July 2012

Mashujaa wa Kenya 'Mau mau' watinga mahakamani jijini London

Group of people detained during the Mau Mau uprising


Ombi la raia wanne mashujaa wa uhuru wa Kenya kutaka kukubaliwa kufungua kesi dhidi ya wakoloni wa Uingereza limeanza kusikilizwa katika mahakama kuu ya Uingereza London. Wanne hao ni pamoja na Paulo Nzilu, Wambugu wa Nyingi, Jane Muthoni Mara na jamii ya Susan Ngondi.

Mashujaa hao wa uhuru wa Kenya wanasema serikali ya Uingereza sharti ikiri kwamba maafisa wake walitekeleza dhuluma za kibinadamu katika iliyokua Koloni yake ya Kenya Afrika Mashariki.

Wamesema kwamba serikali ya ukoloni katika miaka ya hamsini ilitangaza sheria ya hatari ambapo pia Vuguvugu la mau mau lilitangazwa kua la kigaidi na raia walioshukiwa kuwa wanachama walipelekwa katika vizuizi.

 
Wanavijiji Wengi kutoka jamii za Gikuyu, Embu, Meru na Kamba walikamatwa na maafisa wa kikoloni kwa kushukiwa kuunga au kuua wanachama wa Mau Mau na kuwekwa kizuizini ambapo walipitia dhuluma zikiwemo wanaume kuhakisa, ubakaji wa wanawake na mateso mengine.

Chini ya sheria za Uingereza, mtu hawezi kuwasilisha kesi katika mahakama zake inayohusisha matukio yaliyofanyika zaidi ya miaka sita. Hata hivyo mahakama inaweza kuridhia kesi iliyopita miaka sita kusikilizwa kulingana na uzito na matukio ya kesi hiyo.

Mashujaa wa Mau mau wamesisitiza kwamba dhuluma walizopitia ziangaziwe chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu ambayo ilichunguza kesi katika mauaji ya Ki- Nazi pamoja na uhalifu wa kivita kufuatia vita vya uliyokua muungano wa Kosovieti.

Baada ya hoja hizi Mahakama kuu ya Uingereza itaamua ikiwa wazee hawa wanaweza kufungua kesi dhidi ya serikali ya Uingereza kufuatia dhuluma wakati wa harakati za Uhuru.

Kizaa zaa cha nani baba mzazi wa Diamond chaibuka!!


Nasib Abdul 'Diamond'


Siku chache baada ya mzee Abdul Juma kufunguka kuwa yeye ndie baba mzazi wa mwanamuziki nyote nchini Tanzania, Diamond na kusema ya kuwa mwanaye huyo hamthamini toka amepata mafanikio, sasa kumeibuka watu waliodai wao ni ndugu wa tumbo moja na mkali huyo wa muziki wa kizazi kipya wameibuka na kusema baba mzazi wa Diamond alishafariki dunia mwaka 2004.

Baada ya kutokea kwa habari hizo mpya mwandishi wa habari hii aliingia mzigoni ili kupata kujua ukweli halisi wa habari hii, na mtoa habari hizo alikuwa na haya ya kusema “Jamani nyie mmeandika baba wa Diamond ni mzee Abdul Juma, mbona tunavyojua sisi, baba wa Diamond anaitwa Salum Idd na alishafariki dunia tangu mwaka 2004, kama mnataka ukweli zaidi fuatilieni,” alisema mtoa habari huyo na kuahidi kutoa ushirikiano.

Kazi ya kufuatili habari hiyo ilianza na mnao Julai 12, mwaka huu walifanikiwa kutinga nyumbani kwa msichana aliyedai ni dada kwa baba mmoja na Diamond. Msichana huyo anaishi Kariakoo, jijini Dar es Salaam na mdogo mwingine wa Diamond aitwaye Idd Salum ambaye naye anaimba kama kaka yake.

Baada ya salamu za hapa na pale na mapaparazi wetu kujitambulisha kwa familia hiyo, lilifuata swali kama kweli wao ni ndugu wa damu moja na Diamond.


Bwana Abdul Juma ambaye anasema yeye ndie baba mzazi wa Diamond


 Idd: “Mbona kila kitu kipo wazi, hata yule mzee Abdul Juma anaelewa kila kitu kwamba sisi na Diamond ni ndugu, Diamond ni kaka yetu na amekuwa akinisaidia mimi katika shida na raha, baba yetu alishafariki dunia tangu mwaka 2004.

 “Yeye (Abdul) ni baba mlezi tu na anafahamu wazi kuwa yeye ni baba mlezi wa Diamond na kwamba baba yetu alishatutoka.”

Kwa mujibu wa mdogo huyo wa Diamond, Idd, mwaka 1989, mama Diamond (Sanura Khassim ‘Sandra’) alipewa ujauzito na Salum (baba yake) kisha waligombana na kuachana.

 Akasema baada ya kuachana, mama Diamond alikutana na Abdul ambaye alikubali kuwa naye kimapenzi na kuulea ujauzito huo wa mtoto (Diamond).

 Idd akasema Diamond alipozaliwa, Abdul aliendelea kumlea mpaka alipofikisha miaka sita ndipo aliporudi Kariakoo kwa baba yake mzazi (Salum) hadi alipokuwa mtu mzima.

 Akaongeza: “Alipokuja hapa, tuliendelea kuishi naye hadi alipopata uelewa wa kuanza kufanya shuguli zake za muziki ilikuwa ni hapahapa.”

 Kwa upande mwingine, Idd alisisitiza kuwa siku zote anamtambua mzee Abdul kama baba mlezi wa Diamond ingawaje pia anautambua mchango wake kwa kumlea ndugu yake huyo lakini akasisitiza kuwa Abdul siye baba mzazi wa nyota huyo.

 Kijana huyo aliendelea kuweka wazi kwamba, kwa upande wa baba yao huyo marehemu, walizaliwa sita lakini kwa mama tofautitofauti.

Aidha, Idd hakusita kuweka wazi ni kwa nini kaka yake anatumia jina la baba mlezi, Abdul badala ya lile la baba mzazi, Salum. “Kutokana na Abdul kumlea Diamond tangu akiwa tumboni kwa mama yake na pia ndiye aliyempa jina la Nasibu ndiyo maana akaendelea kulitumia jina la baba mlezi maana lipo hata kwenye cheti chake cha kuzaliwa, hivyo ilikuwa vigumu kubadilisha,” alisema.

 Kama madai hayo ni sahihi, ina maana yule msanii wa Bongo Fleva, Mwanahawa Abdul Juma ‘Queen Darleen’ ambaye wengi wanajua yeye na Diamond ni damu moja kwa baba, kumbe hawana uhusiano wowote ule.

Kwa sababu kama mzee Abdul Juma alilea ujauzito wa Diamond lakini damu si yake huku ikijulikana wazi kwamba yeye ni baba mzazi wa Queen Darleen, kwa hiyo Diamond hachangii popote na msanii huyo wa kike.

Kijana huyo aliendelea kutiririka kuwa, maisha yao na Diamond ni safi kwani kunapotokea tatizo lolote, msanii huyo anashiriki kikamilifu na kila Mwezi Mtukufu wa Ramadhan unapowadia, staa huyo huwa anakwenda kufuturu Kariakoo hadi mfungo unapoisha.

Baada ya maelezo hayo ya Idd, kwa mara nyingine mapaparazi wetu walimtokea mzee Abdul Juma anayedaiwa ni baba mlezi tu na kumwambia kila kitu kuhusu maneno yaliyotoka kinywani kwa Idd.

 Mzee Abdul: “Nilijua tu kwamba kuna watu wataibuka wakidai Diamond ni mtoto wao. Hii yote ni kwa sababu ya mafanikio aliyonayo kwa sasa, ukweli ni kuwa yule ni mwanangu wa damu, halali kabisa. Hao wanaosema ni mtoto wao, ni matapeli.”


 Katika hali ya kawaida, mama Diamond (Sandra) ndiye mwenye uhakika wa baba wa mtoto huyo, hivyo Julai 12, 2012, mapaparazi wetu walifika nyumbani kwake, Sinza-Mori, Dar ili kumsikia anasemaje kuhusu hilo.

 Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke huyo hakuwa tayari kujibu swali lolote kuhusu Abdul Juma wala Salum Idd.

 “Sitaki kusema. Sitaki kujibu chochote. Kwa nini msimuulize Diamond, mimi na vyombo vya habari wapi na wapi jamani? Muulizeni mwenyewe Diamond.

 Paparazi: Lakini unawafahamu hawa watu, mzee Abdul na…”

 Mama Diamond: (huku akiangalia ukutani) nimesema sijibu chochote. Kwa nini sieleweki?

Baada ya majibu ya kuzodoa ya mama huyo, Diamond alipigiwa simu, lakini kama ilivyokuwa kwenye habari ya kwanza ya BABA DIAMOND AIBUKA, ANENA MAZITO ambapo alipigiwa simu mara kumi na mbili lakini hakupokea, safari hii pia hakupokea licha ya kutwangiwa mara kadhaa.

 Mpaka gazeti hili linakwenda kukatiza mitamboni, jitihada za kumpata Diamond kuongelea jambo hilo ziligonga mwamba. Hata hivyo, jitihada za kumpata msanii huyo mwenye mafanikio makubwa Bongo zinaendelea.

Source: GPL

Monday, 16 July 2012

Mario Balotelli's mum is cleaner at car lease firm


: Mario Balotelli's mum Rose Barwuah

He earns £120,000 a week, likes to drink vintage champagne straight from the bottle and once famously put hundreds of pounds on to a church collection plate.

But Mario Balotelli's generosity doesn't appear to extend to his mother, who works as a cleaner in an office only a few miles from her son's £3million mansion.

While the Manchester City footballer glides around in his gleaming £120,000 Bentley Continental GT, Rose Barwuah has a more humble mode of transport – the number 11 bus.

Five times a week, she catches the bus to start her job as a cleaner at a car lease firm on the outskirts of Cheadle, near Manchester, earning little more than the minimum wage of £6.08 an hour.

Home for her is a council home in Wythenshawe, the area used to film Shameless, the Channel 4 comedy about feckless families living on benefits.

Accident: Mario Balotelli and his white Bentley which was involved in a crash today
Mario Balotelli and his white Bentley

The 46-year-old gave Balotelli up for adoption when he was two, and she and her husband were living in poverty in a tiny flat in Brescia, Italy.

Last Christmas she moved to the Manchester area to be near her notoriously eccentric son, now 21.

A source said: 'When she came over from Italy with her daughter, Rose, she said she wanted to be close to her son and didn't want any of the huge wealth or luxury he now enjoys.

'And it appears she is staying true to her word, living within her limited means and working hard. It is hard work she is doing but she previously worked in a market so she is pretty tough.

'Mario doesn't live very far away in Alderley Edge but it is a world away as far as lifestyle.'

He added: 'His mother keeps a low profile – she doesn't want Mario to feel pressured by her being in the UK. She just wants to rebuild her relationship with her son as any mother would want.'

Balotelli has visited his mother on several occasions at her small semi-detached home, parking his white Bentley outside.

She and her husband Thomas, who are originally from Ghana, were advised to give him up when he was two because he had a life-threatening intestinal condition made worse by their cramped living quarters.

His mother later claimed the Balotelli family, who adopted Mario, had turned him against his birth relatives and she had to work hard to build a relationship with him.

She recently said: 'Mario has been over to see me a few times. We don't see each other all the time as he has his life and I have mine.'



Picha na video: Raia wa Israel ajichoma moto kwa kulalamikia ugumu wa maisha nchini humo


Moshe Silman baada ya kuokolewa

Raia mmoja wa utawala wa Kizayuni wa Israel amejichoma moto kwenye maandamano yaliyofanyika Tel Aviv kulalamikia ughali mkubwa wa maisha katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Moshe Silman (57) alijimwagia mafuta ya taa na kujichoma moto siku ya Jumamosi na hivi sasa yuko katika hali mbaya kwenye hospitali ya Sheba, baada ya mwili wake kuungua kwa asilimia 90.

Moshe Silman ameamua kujichoma moto baada ya kufilisika na kupoteza matumaini katika maisha kutokana na mfumo mbovu wa kiuchumi wa Israel.


Moshe Silman akiungua, huku baadhi ya waandamanaji wakijaribu kumuokoa kwa kuuzima moto huo


Mwaka 2000 alitumbukia kwenye madeni mazito ya bima yake na huo ulikuwa ni mwanzo tu wa masaibu yake ya kiuchumi.

Kabla ya kujichoma moto, Mzayuni huyo aliandika barua akisema kuwa viongozi wa Israel wanawaibia maskini na kuwatajirisha zaidi matajiri.

Video:

Picha na video: Amir Khan agaragazishwa ulingoni na Danny Garcia


  • Achapwa kwa 'knock out' katika raundi ya nne

Pain game: Carl Froch believes Amir Khan should call it quits after his devastating defeat to Danny Garcia
Khan baada ya kichapo

Ndoto za mwanamasumbwi wa Uingereza Amir Khan zimefika njia panda baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa kijana chipukizi katika masumbwi Danny Garcia wa Marekani anayeshikilia taji la WBC.

Garcia bila kutarajiwa na wengi alimnyuka bingwa wa taji la WBA katika raundi ya nne na kuendeleza sifa yake ya kutoshindwa tangu kuingia katika mchezo wa masumbwi ya kulipwa.

Licha ya kushindwa  katika mchezo huo, Amir Khan alimjeruhi Garcia kunako raundi ya pili akionekana kudhibiti mchezo vizuri raundi zote mbili.

Lakini Garcia alibadilika katika raundi ya tatu na zikisalia sekunde chache kabla ya kengele ya mapumziko, Khan alishangaa kuona mgongo umenyooka kwenye sakafu baada ya konde lililomponda nyuma ya sikio la upande wa kulia. Baada ya hapo ikawa ni mshike mshike, Khan akitafuta kimbilio hadi kipenga kilipopigwa kumnusuru makonde ya mfululizo.

Mwanzoni mwa raundi ya nne, Khan alionekana kupunguza vimulimuli vilivyomzonga mapema kwa makonde ya Garcia lakini alidondoshwa tena kwa konde la Garcia la mkono wa kushoto ulioonekana kumgusa utosi na kumgaragaza chini akakaa kitako.

Ingawaje Khan aliinuka na kurusha makonde yake mazito, mkono wa kushoto wa Garcia ulikipata kichwa cha Khan na kurejesha chini. Aliweza kusimama ingawa miguu ilionekana kama isiyoweza kunyooka kumwezesha kuhimili makonde mazito ya mpinzani wake.

Refa wa mchuano huo Bayless alichukuwa uwamuzi baada ya kumtazama usoni kwa makini na macho yaliyoonekana kuchoka akaamuwa pambano liishie hapo.

Ni hivi karibuni tu Amir Khan karejeshewa mikanda yake baada ya Lamont Peterson wa Marekani kupatikana kua alitumia dawa ya kuongezea nguvu mwili.


Baada ya pambano, Khan alisema haikuwa bahati yangu usiku huu.

Garcia kwa upande wake ulikuwa usiku wa furaha na sherehe baada ya kushinda mikanda yote miwili, WBC na WBA akizidi kuimarisha rekodi yake ya ushindi wa mapambano 24 bila kupoteza pamoja na ushindi wa mara 15 kwa knock out. Khan ameshiriki michuano 26 kashindwa mara tatu ingawa amewahi kushinda 18 kwa kuwakwaza wapinzani wake.

Amir Khan alisema atainuka na kurudi ulingoni na kutaraji kuwa Garcia atawapa fursa ya pambano la marudiano nchini Uingereza. Lakini Babake Garcia hakusita kupinga ombi la Khan kwa kusema, 'khan alimdharau sana mwanangu, kwanini tumpe fursa, ya nini? Hatuwezi kumpa fursa kama hiyo, alisema mzee Angel Garcia.

Picha:
Out of the game: Garcia thunders a right hand at Khan before beating the Briton in Vegas
Konde la kulia la Danny Garcia likimtikisa Amir Khan

Down and out: Khan travels to the canvas in the decisive fourth round
Khan akienda chini bila ya kujitambua

Fall guy: Garcia stands over Khan after delivering a knockout blow in the fourth round
Ngoma ngumu: Khan akipapatua kuinuka katika raundi ya nne

What next? Khan will now contemplate his future after losing his title fight
Khan akifarijiwa na mkufunzi wake baada ya kichapo

King of the ring: Garcia climbs the ropes to celebrates his stunning victory
Danny Garcia akiwa kapanda kamba za ulingo kusheherekea ushindi wake dhidi ya Amir Khan

Video: