Msaada wako unahitajika

Mchango wako unahitajika kuchangia kununua hili Temple na kulifanya kuwa shule ya kiislamu hapo Leicester mjini (Leicester Town Centre). Jengo lina sehemu kubwa kabisa (Hall) ya kufanya msikiti. Inshaallah tukifanikiwa itakuwa ndio msikiti wa kwanza kuwa Town Centre hapa Leicester. Toa kwa ajili ya Allah, chochote utakachotoa ni sawa na sadakat jariya kwani malipo yake yataendelea hata kama utakuwa umetangulia mbele ya haki. Jazakallah Khayr Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi: madrasatulnoor.01@gmail.com

Saturday, 31 December 2011

Picha: Mechi za kufungia mwaka katika ligi kuu Uingereza

Robin van Persie scores for Arsenal against QPR
Ruben Van Parsie akiifungia Arsenal goli pekee katika mchezo wao dhidi ya Queens Park Rangers. Hilo lilikuwa goli la 50 kwa Van Parsie kwa klabu pamoja na timu ya Taifa kwa mwaka huu wa 2011
 
Van Parsie akishangilia goli lake dhidi ya QPR. Mchezo huo ulimalizika kwa Arsenal kushinda kwa goli 1 - 0
 
Stephen Ireland scores for Aston Villa
Stephen Ireland akiisawazishia goli timu yake ya Aston Villa dhidi ya Chelsea. Mchezo huo uliochezwa Stamford Bridge ulimalizika kwa Aston Villa kuifunga timu ya Chelsea goli 3 - 1
 
Crisp strike: Stiliyan Petrov fires Aston Villa intot he lead
Petrov wa Aston Villa akiifungia timu yake goli la pili dhidi ya Chelsea
 
Sealing the deal: Darren Bent makes it 3-1 to ensure Villa take home all three points
Darren Bent akikamilisha goli la tatu na la ushindi dhidi ya Chelsea.
 
Grant Hanley scores the winner for Blackburn
Grant Hanley akishangilia goli lake na la ushindi wakati timu yake ya Blackburn Rovers ilipoibuka na ushindi dhidi ya Manchester utd katika uwanja wa Old Trafford. Blackburn walishinda 3 - 2
 
Head down: A dejected Ferguson makes his way back to the changing room after losing to Blackburn
Alex Ferguson baada ya mchezo kati ya Manchester united na Blackburn, ambapo Manchester walifungwa goli 3 - 2
 
Timing: Rafael van der Vaart shows great technique to turn the ball home just before the break
Breakthrough: Rafael van der Vaart is given a lift by Benoit Assou-Ekotto after scoring Spurs' opener
Juu Rafael Van de Vaart wa Tottenham akiifungia timu yake goli la kuongoza dhidi ya Swansea na chini yake wachezaji wenzake wakimpongeza.
 
Scott Sinclair celebrates with Kemy Agustien and Stephen Dobbie
Scot Sinclair wa Swansea (kati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli la kusawazisha dhidi ya Tottenham. Mchezo huo ulimaliza kwa sare ya 1 - 1
 
Orlando Sa wa Fulham akishangilia goli lake aliloifungia timu yake na meneja wake Martin Jol. Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1 - 1
 
Simeon Jackson
Jackson wa Norwich akishangilia goli lake la kusawazisha dhidi ya Fulham katika dakika za majeruhi. Mchezo huo ulimaliza kwa sare ya goli 1 - 1
 
Steven Gerrard scores Liverpool's third goal
Steven Gerrard wa Liverpool akiifungia timu yake goli la tatu dhidi ya Newcastle. Mchezo huo ulimaliza kwa Liverpool kushinda goli 3 - 1
 
Liverpool manager Kenny Dalglish delighted with return of Steven Gerrard
Steven Gerrard akishangilia goli lake dhidi ya Newcastle pamoja na meneja wake Ken Daglish

Uncle Roy Sr anawatakia heri ya mwaka mpya


Matokeo ya ligi kuu nchini Uingereza: Mechi za kumalizia duru la kwanza na kufungia mwaka 2011

FT Manchester U. 2 - 3 Blackburn R.
FT Arsenal 1 - 0 Queens Park R.
FT Bolton W. 1 - 1 Wolverhampton W.
FT Chelsea 1 - 3 Aston Villa
FT Norwich C. 1 - 1 Fulham
FT Stoke C. 2 - 2 Wigan Athletic
FT Swansea C. 1 - 1 Tottenham H.

Nimeipenda hii


Moja ya majengo maarufu jijini Leicester nchini Uingereza

Ligi kuu Uingereza: Chelsea yatolewa nishai Stamford Bridge

  • Yafungwa 3 - 1 na Aston Villa kwao
Up and running: Didier Drogba hits his 150th goal for Chelsea
Drogba akifunga penati na kuipatia Chelsea goli la kuongoza, na pia kuifungia Chelsea goli lake la 150, tangu alipojiunga na timu hiyo

Timu ya Chelsea ya London leo imepata kibano cha bao 3 - 1 kutoka kwa timu ya aston Villa katika mchezo wa kukamilisha duru la kwanza la ligi kuu nchini Uingereza, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa timu ya Chelsea wa Stamford Bridge.

Chelsea ndio walikuwa wa kwanza kujipatia bao kunako dakika ya 23 lililofungwa na mshambuliaji wao mahiri Didier Drogba kwa njia ya penati.

Dakika tano baadae Stephen Ireland aliisawazishia Aston Villa baada ya kutokea kizaa zaa golini mwa Chelsea baada ya John Terry kuokoa hatari golini humo na kumkuta mfungaji huo na kuujaza wavuni.

Charles N'Zogbia and Stephen Ireland - Chelsea v Aston Villa match report
Charles N'zogbia akimpongeza Stephen Ireland baada ya kufunga goli la kusawazisha

Kipindi cha pili Chelsea waliutawala mchezo huo lakini bahati haikuwa yao, kwani mnamo dakika ya 83 nahodha wa Villa Stilian Petrov aliipatia timu yake bao la pili baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ciaran Clark ambayo ilifanya walinzi wa kati wa Chelsea kuchelewa kuwa katika nafasi zao.

Darren Bent ambaye alikosa mechi tatu za Villa kutokana na kuumia aliipatia timu yake bao la tatu kunako dakika ya 87.

Disappointing defeat: Andre Villas-Boas saw his side beaten in their final game of 2011
Meneja wa Chelsea na benchi lake la ufundi wakiwa hawaamini nini kimetokea

Kwa matokeo hayo timu ya Chelsea inamaliza mwaka huu ikiwa katika nafasi ya tano katika ligi kuu ya Uingereza.


Video: Petrov akifunga goli la pili dhidi ya Chelsea

Mtuhumiwa wa wizi wa Mbuzi akatwa sikio na kulazimishwa kulila kwa kutolea chumvi



Mkazi wa mtaa wa Maisaka Sinai mjini Babati mkoani Manyara, amenusurika kuuawa baada ya kukatwa sikio na kulazimishwa kulimeza kutokana na kipigo cha kwa wananchi, akidaiwa kuiba mbuzi wawili na kutaka kuwauza.

Daatho Kodi (20) alipigwa na wananchi siku ya Jumatano saa 10 jioni, kwenye mnada wa Gendi wilayani Babati na kukatwa sikio la kushoto na kulazimishwa kulitafuna akipewa na chumvi.

Akizungumza kwa njia ya simu,mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Joseph Muray ambaye alikuwa mnadani hapo, alisema kama si jitihada za Mwenyekiti wa soko hilo, Sifael Mollel, hivi sasa Kodi angekuwa marehemu.

Muray alisema Mollel alitumia askari wa mgambo mnadani kuzuia vurugu hizo na kuwaita polisi waliofika eneo hilo wakati Kodi ameshajeruhiwa kwa kipigo na kukatwa sikio.

Alisema watu hao walimpiga mtuhumiwa huyo aliyedaiwa kuiba mbuzi wawili, beberu na jike, mali ya Safari Angali (24) mkazi wa mtaa wa Nakwa Barazani, Babati.

Alisema baada ya kuiba mbuzi hao aliwapeleka mnadani hapo na wakati akitafuta mnunuzi, alikamatwa na kupigwa kwa silaha za jadi.

Muray alisema alipokamatwa aliambiwa achague moja, kati ya kuuawa au kukatwa sikio na
kulitafuna na chumvi na kulimeza, akachagua sikio likatwe.

“Alipigwa kwa marungu na mapanga na kukatwa sikio na kupewa chumvi na kulitafuna na kulimeza hadi polisi walipoitwa,” alisema shuhuda huyo.

Alidai kuwa, Kodi ni mzoefu wa kuiba mali za watu na amekuwa akikamatwa na kuachwa kutokana na kulindwa na ndugu na jamaa zake.

“Walitaka kumuua na kama si Mwenyekiti kuita polisi wangemmaliza, kwani walidai wakimkamata huachiwa,” alisema.

Kodi anaendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara) huku akiwa na pingu mikononi.

Ligi kuu Uingereza: Manchester United yapewa kibano kwao

  • Yafungwa 3 - 2 na Blackburn Rovers
Cool head: Yakubu slams home his penalty to give Blackburn the lead against Manchester United
Yakubu akifunga goli kwa njia ya penati

Magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa Blackburn Rovers Yakubu na la kichwa lilifungwa na Grant Hanley yametosha kuipa timu ya Blackburn ushindi wa goli 3 - 2 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza Manchester United.

Blackburn wakiwa wanacheza mchezo huo wa kukamilisha duru la kwanza la ligi hiyo wakiwa wageni wa Manchester utd, walijipatia goli la kwanza kwa njia ya penati iliyofungwa kiufundi na Yakubu katika dakika ya 16, baada ya mshambuliaji wa Manchester utd Dimitar Berbatov kumvuta fulana na kumuangusha mlinzi wa Blackburn Chris Samba.

Mpaka mapumziko Blackburn walikuwa wakiongoza kwa goli 1 - 0.

Birthday blues: Yakubu gave Blackburn a shock lead from the penalty spot
Wachezaji wa Blackburn wakishangilia goli lililofungwa na Yakubu

Kipindi cha pili kilianza kwa Manchester kufanya mabadiliko ya kumpumzisha mshambuliaji wake Javier Harnandes na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji wa kiungo Anderson. Lakini ilikuwa ni Blackburn waliojipatia goli la pili mnamo dakika ya 51 lililofungwa na Yakubu.

United iliwachukuwa dakika moja tu baada ya Yakubu kufunga goli la pili, na kujipatia goli lao la kwanza lililofungwa na Dimitar Berbatov, mchezaji huyo huyo aliipatia Untied bao la kusawazisha mnamo dakika ya 62.

Lakini hiyo haikutosha kwani mnamo dakika ya 80 Grant Hanley aliifungia Blackburn goli la ushindi kwa kichwa kutokana na kona iliyopigwa na Morten Gamst Pedersen na baada ya kipa wa Manchester kutoka golini kuupiga ngumi mpira huo na kuukosa.

Blackburn Rovers' Grant Hanley celebrates
Grant Hanley akishangilia goli la tatu na la ushindi dhidi ya Manchester utd

Kwa matokeo hayo timu ya Manchester United itaanza mwaka mpya wakiwa katika nafasi ya pili na Manchester City bado wakiwa killeleni.

Ama kweli pombe kumbe sio chai!!

,,.HII STYLE INAITWAJE!!!!!!!!!!!!!!!!

Sijaifahamu hii si style gani na ya wapi!!

Ligi kuu Uingereza: Mechi za kumaliza duru ya kwanza na kufunga mwaka

December 31
 13:45 Manchester U.  - Blackburn R.
15:00 Arsenal  - Queens Park R.
15:00 Bolton W.  - Wolverhampton W.
15:00 Chelsea  - Aston Villa
15:00 Norwich C.  - Fulham
15:00 Stoke C.  - Wigan Athletic
15:00 Swansea C.  - Tottenham H.

Carlo Anchelotti ateuliwa kuwa kocha mpya wa Paris St-Germain

Carlo Ancelotti's appointment as new Paris St-Germain coach is a clear statement of intent by French club
Carlo Anchelotti

Baada ya miezi saba kuwa nje ya kazi tangu alipofukuzwa kazi ya kuifundisha Chelsea na tajiri wa timu hiyo Roman Abromavic, Carlo Anchelotti amchaguliwa kuwa kocha wa timu Paris St-Germain  inayoshiriki ligi kuu nchini Ufaransa.

Anchelotti mwenye umri wa miaka 52 amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na inasemekana atakuwa analipwa kiasi cha paundi milioni 5 kwa mwaka.

Paris Saint Germain (PSG) new coach Carlo Ancelotti holds a team jersey after a press conference. Photo / AP

Timu hiyo ambayo mmiliki wake ni Qatar Sports Investments ambao wapo tayari kutumia mamilioni ya paundi kwa ajili ya kuimarisha timu hiyo. Tayari walishamnunua kiungo wa Argentina Javier Pastore kwa kiasi cha milioni £75.5

Siku ya Jumapili ambako soko la kununua wachezaji litafunguliwa tayari timu hiyo inategemewa kusajili wachezaji wengine kama Kaka kutoka Real Madrid, Alexandre Pato kutoka AC Milan na hata David Beckham kutoka Los Angeles Galaxy ya Marekani.

Arsene Wenger - I only bring back special players

Thierry Henry of the New York Red Bulls during an Arsenal training session at London Colney
Thierry Henry during an Arsenal training session at London Colney, on Friday

It takes an exceptional breed of player to return to Arsenal, according to Arsène Wenger.

Wenger confirmed on Friday that Thierry Henry is likely to re-join the Club on a two-month loan spell from New York Red Bull, returning to Emirates Stadium after four years away.

Henry is set to follow in the footsteps of Sol Campbell and Jens Lehmann, who re-joined on short-term deals in recent seasons. Wenger believes experience at this stage of the campaign is invaluable.

"I never did it before,” he said. “You must have noticed that I only do it on short term.

I know him so well: Wenger (right) with Henry at Friday's training session

“I've done it with players who have a special attitude, special weight in the dressing room and I've done it at periods where experience can play a big part in the dressing room, from January to March.

"Before I did it with a very young side and you can feel that when it comes to March they get a bit nervous. Players who have won before can help them keep calm.

“Now I do it for footballing reasons because I need a striker for two months.”

Campbell, like Henry, made his Arsenal return in January 2010 after four years away. Wenger believes the duo share rare qualities that convince him they can still offer something.

"Sol was fantastic when he came back,” he said. “Sol is like Thierry. Once they are committed you know you can rely on them.

"I remember when we went to Tottenham, Sol was absolutely amazing for a guy who, three weeks before, you wondered if he could still play in the Premier League.

"He had such a capacity to fight and it's important to bring that out. They have that pride. When players play they will want to be good.”

Ligi kuu Uingereza: Liverpool 3 - 1 Newcastle


Steven Gerrard akishangilia goli lake na meneja Ken Daglish

Magoli mawili yaliyofungwa na Craig Bellamy na moja kutoka kwa nahodha Steven Gerrard yameifanya timu ya Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 3 - 1 dhidi ya timu ya Newcastle.

Newcastle ndio walikuwa wa kwanza kujipatia goli ambalo lilifungwa na mlinzi wa kati wa Liverpool Daniel Agger baada ya kubabatizwa na mpira wa krosi uliopigwa na Ryan Taylor mnamo dakika ya 25.


Bellamy akishangilia goli lake la kwanza

Craig Bellamy aliisawazishia timu yake goli mnamo dakika ya 29 kwa shuti la chini, mpira ambao ulipigwa krosi na mlinzi Jose Enrique na kumkuta Charlie Adam kisha kumgonga Gutierrez na mpira huo kumkuta Bellamy ambae aliunganisha moja kwa moja mpaka nyavuni.

Mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa sare ya goli 1-1.


Bellamy akifunga goli lake la pili kwa njia ya adhabu ndogo

Craig Bellamy alijiaptia goli la pili la mchezo na la pili kwa timu yake mnamo dakika ya 67 kwa mpira wa adhabu ndogo ambao aliupiga na kwenda moja kwa moja golini huku akiwacha mlinzi wa Newcastle na kipa wake wakibabatizana.

Nahodha wa Liverpool Gerrard ambaye alichukuwa nafasi ya Charlie Adam aliipatia timu yake bao la tatu na la ushindi katika dakika ya 77.


Wachezaji wa Liverpool wakishangilia goli lao la tatu

Kwa ushindi huo Liverpool imefikisha pointi 34 baada ya kukamilisha michezo yake ya duru la kwanza la ligi hiyo, na kushika nafasi ya tano.

Upotevu wa dola 50000 mikononi mwa polisi jijini Arusha

  • Askari baada ya kupatiwa dhamana, atoweka pamoja na familia yake


Mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania Said Mwema.

Askari Polisi anayedaiwa kuhusika na wizi wa dola za Marekani 50,000 za kidhibiti katika kituo kikuu cha Polisi jijini Arusha, ametoroka na familia yake.

Askari huyo (jina limehifadhiwa) anadaiwa kutoroka usiku wa manane wakati Tume maalumu ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, ikiwa inaendelea kuhoji polisi na raia juu ya upotevu wa fedha hizo.

Awali askari huyo, aliwekwa rumande na mwenzake, lakini walipewa dhamana baada ya kuandika
maelezo kwa viongozi hao wa juu wa Polisi mkoani hapa juu ya wizi huo.

Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa, alipoulizwa alikiri kuwekwa ndani kwa askari hao, lakini alikataa kutaja majina yao kwa sababu za kichunguzi juu ya suala hilo.

Mbali ya askari huyo kutoweka, askari kanzu mwingine mwenye cheo cha Konstebo (jina tunalo), alikamatwa juzi jioni na anashikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi kwa madai ya kufahamu mtandao mkubwa wa wizi jijini hapa na kuhusika na wizi wa fedha hizo.

Mpwapwa alipoulizwa jana kwa njia ya simu juu ya kutoweka kwa askari huyo na familia yake, na mwingine kukamatwa, alisema yeye yuko nje ya mji, labda inawezekana ikawa kweli au la, lakini kwa kuwa yuko nje ya ofisi hilo hatalizungumzia.

‘’Mimi niko Karatu kikazi labda huyo askari alitoroka wakati nikiwa huku na kama kuna mwingine, nikirudi kesho (leo) nitapata taarifa kwa ukaribu zaidi na kupata ukweli wake,’’ alisema Mpwapwa.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, kukamatwa kwa askari kanzu huyo kulitokana na taarifa kutoka kwa raia wema kuwa askari huyo alihusika moja kwa moja na upotevu wa dola hizo.

Habari zilisema kuwa konstebo huyo piaanadaiwa kumiliki magari ya kisasa jijini Arusha, zaidi ya 10 yakiwamo yaliyokodishwa na mengine kubeba abiria - teksi.

Vyanzo vya habari vilisema kwamba baadhi ya askari kanzu ambao wanafanya kazi karibu na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Arusha (RCO) ambao walikuwa zamu siku ya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa nao tayari wamehojiwa na Tume hiyo ya IGP.

Fedha hizo za kigeni sawa na Sh milioni 90 zinazodaiwa kuwa sehemu ya dola za Marekani 200,000 zilizoporwa zilioneshwa mahali ziliko na mmoja wa watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na ujambazi wa kutumia usafiri aina ya pikipiki maarufu jijini Arusha kwa jina la Toyo ama Bodaboda.

Fedha hizo dola 50,000 ziliyeyukia mikononi mwa polisi katika mazingira ya kutatanisha.

Watuhumiwa hao wa ujambazi walifanya uhalifu huo hivi karibuni kwa kumpora dereva wa gari la hoteli maarufu ya kitalii ya jijini hapa ya Kibo Palace, Onesmo Joseph (28), dola 200,000 sawa na zaidi ya Sh milioni 340.

Thursday, 29 December 2011

Kituko hiki

INGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE?

Miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika; hali za barabara zetu ndio kama hivi!!


Hali hii tuifahamu vipi? Wapo wapi wabunge wa maeneo haya? Ziko wapi wizara na idara husika? Au kwa kuwa viongozi wa juu wa serikali hawazitumii barabara hizi?
Source: Mbeya yetu

Nimeipenda hii


Hii inaitwa "Full kufunga au full kuuramba"

Chuo Kikuu cha Zanzibar chakubaliana na chuo kikuu cha Indiana cha Marekani



Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) pamoja na Chuo Kikuu cha Marekani cha Indiana, vimetiliana saini makubaliano ya kuimarisha na kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni Zanzibar.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika chuo hicho kati ya Makamu Mkuu wa Suza, Profesa Idrissa Ahmed Rai na Mkuu wa Kitivo cha Kiswahili cha Chuo Kikuu cha Indiana cha Marekani,
Alawia Omar.

Professa Rai alisema mikakati ya SUZA ni kuhakikisha kwamba Kiswahili kinaongeza wigo wa
kufundishwa kwa watu mbalimbali.

“Tumefurahishwa na mipango ya ushirikiano katika kuimarisha Kiswahili kwa kukifundisha kwa watu wa mataifa mbalimbali ulimwenguni,” alisema.

Alisema mikakati ya kukipanua Kiswahili inakwenda sambamba na mipango ya viongozi wa
Umoja wa Afrika wa kutaka lugha hiyo sasa kutumiwa katika taasisi na vyombo mbalimbali vikiwemo vya kutunga sheria.

Naye Alawia alitoa vifaa mbalimbali vya kufundishia Kiswahili kwa ajili ya matumizi ya Suza.

`Maalim Seif amevunja sheria ya katiba mpya`



Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amelalamikiwa kuwa amevunja Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011kutokana na kitendo cha kuwafundisha wananchi mambo ya kuzingatiwa kuwemo katika mfumo wa Muungano.

Hayo yameelezwa na Chama cha National League for Democracy, (NLD) katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa chama hicho, Khamis Haji Mussa.

Alisema kwamba Maalim Seif amevunja kifungu cha 18 cha sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Novemba mwaka huu.

 
Alisema sheria hiyo inakataza mtu au taasisi yoyote kuhamasisha, kushawishi au kufanya kampeni zenye lengo la kuwataka wananchi kufuata matakwa ya chama au mtu katika mjadala wa katiba.

 
Khamis alisema Desemba 24, mwaka huu Maalim Seif aliwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mchakato wa katiba mpya wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kibandamaiti, Zanzibar.

 
“Bahati mbaya, Maalim Seif hotuba yake imewashawishi watu kutenda mambo anayoyataka yeye, kitendo ambacho kinyume na sheria,” alisema Khamis.

Alisema kuwa Zanzibar inaogozwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria, Maalim Seif akiwa kiongozi wa kitaifa hakupaswa kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika mjadala wa katiba mpya ya Muungano.

 
Alisema kwamba chama chake kinaamini Wazanzibari wana akili timamu na wanazijua kero za muungano na wana uwezo wa kuzieleza bila ya kufundishwa na kiongozi au chama cha siasa.

 
Alisema katika mkutano wake Maalim Seif aliwataka wananchi kudai Zanzibar iwe na benki kuu yake, Jeshi la polisi, urais wa Muungano utokane na zamu na kuwe na usawa katika nafasi za ubalozi.

“NLD inavishauri vyombo vya sheria kuifanyia kazi hutuba ya Maalim Seif na sheria ichukuwe mkondo wake,” alisema Khamis.
Alisema wakati huu wa kuelekea mjadala wa katiba mpya siyo jambo la busara kwa vyama vya siasa au asasi za kiraia kuwafundisha wananchi mambo ya kudai katika katiba mpya

Chanzo: Nipashe

Hivi kweli asiyekula nanasi, hajala kitu kitamu?

Nimeipenda hii


Mmoja wa wafanyakazi katika soko kuu la Darajani mjini Unguja akimkata vipande samaki aina ya Nduaro. Inasemekana samaki huyo ameuzwa shilingi laki tano katika mnada uliofanyika sokoni hapo

Ama kweli dunia tambara bovu; Ukishangaa ya Mussa utayaona ya Firauni


Huu ni uzima kweli!!?

Luis Suarez afungiwa mechi moja na faini kwa kuwatukana wapenzi wa Fulham

Liverpool's Luis Suarez given new one-match ban by the FA
Luis Suarez akiwaonyeshea kidole wapenzi wa Fulham baada ya mchezo wao kuisha na Liverpool kufungwa goli 1 - 0

Mshambuliaji wa klabu ya kandanda ya Liverpool, Luis Suarez amefungiwa kucheza mechi moja na kutozwa faini ya paundi za kingereza 20,000 na ameonywa kuchunga tabia yake siku zijazo baada ya kukiri mashtaka yaliyoainishwa na Chama cha Soka cha England FA, juu ya utovu wake wa nidhamu.

Suarez hatacheza mechi ya siku ya Ijumaa Liverpool watakapopambana na Newcastle katika uwanja wa Anfield akiwa anatumikia adhabu hiyo. Amepewa adhabu hiyo mpya ya mechi moja kwa kuonesha kidole cha kati dhidi ya wapenzi wa timu ya Fulham kama ishara ya matusi walipofungwa bao 1-0 na timu hiyo tarehe 5 mwezi huu. Aliinua kidole chake cha kati cha mkono wa kushoto wakati akitoka nje ya uwanja.

Hivi karibuni Suarez alipewa adhabu ya kufungiwa kucheza kandanda mechi nane kutokana na kosa la kumtusi kwa maneno ya kibaguzi mlinzi wa Manchester United Patrice Evra.

Klabu ya Liverpool pia imetozwa faini ya paundi 20,000 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake katika mechi hiyo dhidi ya Fulham. Wachezaji kadha walimzonga mwamuzi Keith Friend wakati kiungo wa timu hiyo Jay Spearing alipooneshwa kadi nyekundu.

Klabu hiyo imekiri makosa yake kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake lakini imepinga adhabu ya faini.

Hata hivyo, tume huru ya maadili imesema adhabu ya paundi elfu 20,000 ni sahihi.

Liverpool ilisema hawana cha kusema juu ya adhabu hiyo ya kufungiwa kwa Suarez ama faini iliyopigwa klabu.