
Wananchi wanaopinga ziara ya Hlary Clinton nchini Misri
Sambamba na wananchi wengi wa Misri kuendelea kupinga uhusiano wowote wa Marekani na nchi hiyo, hii leo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani Hillary Clinton amewasili mji mkuu wa Misri, Cairo.
Katika safari hiyo Clinton anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Muhammad Mursi kuhusu tatizo la madaraka kati ya rais huyo mwenye mielekeo ya Kiislamu na majenerali wa jeshi ambao wanamadaraka makubwa.
Hii ni mara ya pili kwa Hillary Clinton kufanya safari nchini Misri tangu mwaka uliopita. Alkhamisi iliyopita Harakati ya Vijana ya Misri ilitoa tangazo la kupinga safari hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na kuyataka makundi mbalimbali ya kisiasa na ya vijana kufanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani mjini.
No comments:
Post a Comment