Wednesday, 2 May 2012

Jacqueline Wolper: "Uwoya haniwezi na hakuna anaeweza kunitishia maisha"

Jack Wolper


Nyota wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameibuka na kumtambia msanii mwenzake kwenye fani hiyo, Irene Uwoya akisema: “Uwoya haniwezi, hakuna mtu anaweza kunitishia maisha.”

Jacquline Wolper amesema hayo baada ya Irene Uwoya kuzungumzia kuhusu kitendo cha kutokuwepo kwa Wolper msibani ni unafiki, na pia kutishia kuwa atampiga msanii huyo.

Akizungumza wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Wolper alisema tangu amezaliwa hajawahi kupigwa hata na wazazi wake hivyo itakuwa jambo la aibu sana kwake kupigwa ukubwani.

“Hakuna mtu anayeweza kunifanyia lolote, mimi ninajiamini kuliko kawaida. Simuogopi mtu yeyote wala sihofii chochote kwa sababu sijamfanyia mtu ubaya wowote,” alisema Wolper

“Kama Uwoya anaona nimekosea kweli na adhabu yangu ni kipigo, aje anipige, ingawa ninauhakika hawezi kufanya hivyo hapa amefika.”

Katika habari iliyochapishwa tarehe 14/04/2012, Uwoya alieleza sababu tatu za kumpiga Wolper ikiwemo ile ya kusafiri na kuacha maziko ya marehemu Steven Kanumba yakiendelea wakati alikuwa ni mtu wa karibu sana na msanii huyo.

Source: Global Publishers

No comments:

Post a Comment