
Andy Carrol akishangilia goli lake na la ushindi kwa timu yake ya Liverpool
Bao la Andy Caroll katika dakika za lala salama katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Everton katika uwanja wa Wembley, limeipatia Liverpool tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la FA nchini Uingereza.

Luis Suarez akiipatia Liverpool bao la kusawazisha
Makosa ya mlinzi wa Everton Sylvain Distin kutoa pasi kwa kipa wake Tim Howard ambapo mpira huo ulikuwa mdogo ndipo mshabuliaji wa Liverpool Luis Suarez aliitumia nafasi hiyo kwa kuuwahi mpira huo na kuutumbukiza mpira wavuni.
Na ndipo mnamo dakika ya 87 mchezaji ghali wa kingereza Andy Carroll, aiweza kuamsha mayowe ya wapenzi wa Liverpool waliokuwa katika uwanja huo wa Wembley kwa kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Craig Bellamy.
Liverpool sasa imejiweka katika nafasi nzuri ya kuweka mkobani Kombe la FA, baada ya tayari kuweka kibindoni Kombe la Carling.
No comments:
Post a Comment