Irene Uwoya
Baada ya habari za mcheza filamu maarufu wa Bongo Irene Uwoya kuwa na mimba ya nje ya ndoa kuzagaa ndani na nje ya Bongo, mrembo huyo amekuwa akijutia kuwa na ukaribu na jamaa ambaye inasemekana ndiye mwenye mzigo huo ajulikanae kwa jina la Ababuu.
Uwoya ambaye ndoa yake na mcheza soka wa Rwanda Hamad Ndikumana iko katia mashaka, alisema kuwa ukaribu wake na Ababuu ndio uliowapa wabaya wake kuzusha suala hilo la ujauzito.
Uwoya alisema ukaribu kati yake na Ababuu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Jacquline Wolper, ulikuwa ni wa kawaida tu na wa masuala mengine na wala sio kama watu wanavyovumisha kuwa wapenzi.
Alisema "“Kwa kweli najuta kuwa karibu na Ababuu kwani wabaya wangu wameitumia fursa hiyo kuzusha maneno ambayo hayana msingi juu yangu,”
“Wabaya wangu wameitumia fursa ya mimi kuwa karibu na Ababuu kunichafua na laiti ningejua ningeuepuka mapema ukaribu huo,” alisema.
Na alipoulizwa juu ya ujauzito unaozungumzwa mitaani, alikuwa na haya ya kusema: “Wewe unanionaje kwani, nina mimba au sina? Kwa kifupi siwezi kubeba ujauzito nje ya ndoa".
Lakini baadhi ya watu wanasisitiza kuwa kitumbo tayari kimeshaanza kutoka.
No comments:
Post a Comment